Loading...
 

Kuwa Mshauri Kwa Ufupi

 


Imechangiwa na Frank Thorogood

Kamusi ya Oxford imefasili mshauri (mnasihi) kama “ni mtu anayetoa ushari, mwenye uwezo na kuaminika”.

Karibia kila mtu ana silika ya uwoga wa kuzungumza mbele ya hadhira.
Inataka ujasiri kujiunga na klabu, lakini pia mwanachama mpya anakutana na msururu mzima wa utaratibu na desturi/tamaduni ambazo zinatumika kuongoza mikutano ya klabu na kufundisha mpango mzima.
Hii inaweza kuwashinda wanachama wapya lakini ni kitu ambacho kimezoeleka na wenye uzoefu zaidi.
Kwahiyo, jukumu la msingi la kuwa mshauri ni la wanachama wenye uzoefu zaidi wa "kumshika mkono mwanachama mpya", kumuelezea kila kitu ambacho hakipo wazi, na kuwa na nafasi ya kumpa ushauri pale unapohitajika, ikiwemo nje ya mikutano ya klabu.

Tatizo kubwa zaidi ni kupatanisha kwa usahihi mshauri na mshauriwa. Hii ni tatizo hasa kwa klabu mpya.

Haya hapa ni mapendekezo machache ya kufanikisha mpango wa ushauri wa klabu:

  • Kamati ya klabu inatakiwa kuandaa orodha ya washauri wanaoweza. Hawa wanatakiwa kuwa wanachama wenye uzoefu zaidi, au, hata kama klabu ni mpya, wale wenye ujuzi kidogo wa kuzungumza mbele ya hadhira, ualimu, nk., au ambao wameonyesha uwezo fulani wa kuelewa kazi za klabu na malengo.
  • Pale atakapokuwa na makubaliano ambayo yanawezekana ya ushauri, VP wa Uanachama anatakiwa kuandaa na kuwa na orodha inayoonyesha washauri na washauriwa wake, kila mshauri anatakiwa kuwa na washauriwa wasiozidi watatu.
  • Kila mwanachama mpya wa klabu atatakiwa kupewa orodha pale atakapojiunga kwenye klabu, na atatakiwa kuchagua mshauri ambaye bado anapatikana kutoka kwenye orodha hiyo, hata kama watasubiri mikutano michache ili waweze kuwafahamu.
  • Mshauri na mshauriwa wanatakiwa kupeana namba za simu na barua pepe na kuwasiliana pia kwenye mbinu mpya za mawasiliano kama vile Facetime, Whatsapp, Skype, nk.

Wanaweza kukutana kijamii ambapo mshauri anaweza kuelezea mpango wa kielimu na utaratibu wa klabu na majukumu na kujibu maswali yoyote.
Baadaye, mshauri bado anaendelea kuwepo kwenye matukio muhimu ya mshauriwa, kama vile hotuba yake ya kwanza, masahihisho ya lugha, nk.

Hata hivyo, mwanachama mpya hatakiwi kumtegemea sana mshauri na anatakiwa kufanya juhudi kuelewa mpango wa kujifunza na majukumu mbalimbali ya mwanachama kwa kutumia nyenzo ambazo zipo.


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Monday August 16, 2021 14:49:33 CEST by zahra.ak.